21. Kwa ajili ya mambo matatu nchi hutetemeka,Naam, kwa ajili ya manne haiwezi kuvumilia.
22. Mtumwa apatapo kuwa mfalme;Mpumbavu ashibapo chakula;
23. Mwanamke mwenye kuchukiza aolewapo;Na mjakazi aliye mrithi wa bibi yake.
24. Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo;Lakini vina akili nyingi sana.
25. Chungu ni watu wasio na nguvu;Lakini hujiwekea chakula wakati wa hari.
26. Wibari ni watu dhaifu;Lakini hujifanyia nyumba katika miamba.
27. Nzige hawana mfalme;Lakini huenda wote pamoja vikosi vikosi.
28. Mjusi hushika kwa mikono yake;Lakini yumo majumbani mwa wafalme.
29. Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza,Naam, wanne walio na mwendo mzuri.
30. Simba aliye hodari kupita wanyama wote;Wala hajiepushi na aliye yote;