Mit. 30:17-23 Swahili Union Version (SUV)

17. Jicho la mtu amdhihakiye babaye,Na kudharau kumtii mamaye;Kunguru wa bondeni wataling’oa,Na vifaranga vya tai watalila.

18. Kuna mambo matatu yaliyo ya ajabu kwangu,Naam, kuna manne nisiyoyafahamu.

19. Mwendo wa tai katika hewa;Na mwendo wa nyoka juu ya mwamba;Mwendo wa merikebu katikati ya bahari;Na mwendo wa mtu pamoja na msichana.

20. Hivyo ndivyo mwendo wa mwanamke mzinifu;Hula, akapangusa kinywa chake,Akasema, Sikufanya uovu.

21. Kwa ajili ya mambo matatu nchi hutetemeka,Naam, kwa ajili ya manne haiwezi kuvumilia.

22. Mtumwa apatapo kuwa mfalme;Mpumbavu ashibapo chakula;

23. Mwanamke mwenye kuchukiza aolewapo;Na mjakazi aliye mrithi wa bibi yake.

Mit. 30