31. Usimhusudu mtu mwenye jeuri,Wala usiichague mojawapo ya njia zake.
32. Maana mtu mkaidi ni chukizo kwa BWANA,Bali siri yake ni pamoja na wanyofu.
33. Laana ya BWANA i katika nyumba ya waovu,Bali huibariki maskani ya mwenye haki.
34. Hakika yake huwadharau wenye dharau,Bali huwapa wanyenyekevu neema.