2. Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi;Bali mwovu atawalapo, watu huugua.
3. Apendaye hekima humfurahisha babaye;Bali ashikamanaye na makahaba hutapanya mali.
4. Mfalme huithibitisha nchi kwa hukumu;Bali yeye apokeaye rushwa huipindua.
5. Mwenye kujipendekeza kwa jirani yake,Hutandika wavu ili kuitega miguu yake.
6. Kuna mtego katika kosa la mtu mbaya;Bali mwenye haki huimba na kufurahi.