Mit. 29:1-8 Swahili Union Version (SUV)

1. Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo,Atavunjika ghafula, wala hapati dawa.

2. Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi;Bali mwovu atawalapo, watu huugua.

3. Apendaye hekima humfurahisha babaye;Bali ashikamanaye na makahaba hutapanya mali.

4. Mfalme huithibitisha nchi kwa hukumu;Bali yeye apokeaye rushwa huipindua.

5. Mwenye kujipendekeza kwa jirani yake,Hutandika wavu ili kuitega miguu yake.

6. Kuna mtego katika kosa la mtu mbaya;Bali mwenye haki huimba na kufurahi.

7. Mwenye haki huyaangalia madai ya maskini;Bali mtu mbaya hana ufahamu hata ayajue.

8. Watu wenye dharau huwasha mji moto;Bali wenye hekima hugeuzia mbali ghadhabu.

Mit. 29