Mit. 28:1-7 Swahili Union Version (SUV)

1. Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu;Bali wenye haki ni wajasiri kama simba.

2. Kwa sababu ya maasi ya nchi wakuu wake huwa wengi;Bali kwa wenye ufahamu na maarifa hali ya nchi hudumishwa

3. Mtu mhitaji awaoneaye maskini,Ni kama mvua ya dhoruba isiyosaza chakula.

4. Wao waiachao sheria huwasifu waovu;Bali wao waishikao hushindana nao.

5. Watu wabaya hawaelewi na hukumu;Bali wamtafutao BWANA huelewa na yote.

6. Afadhali maskini aendaye katika unyofu wake,Kuliko mpotofu wa njia angawa ni tajiri.

7. Yeye aishikaye sheria ni mwana mwenye hekima;Bali aliye rafiki wa walafi humwaibisha babaye.

Mit. 28