17. Chuma hunoa chuma;Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake.
18. Yeye autunzaye mtini atakula matunda yake;Naye amhudumiaye bwana wake ataheshimiwa.
19. Kama uso ufananavyo na uso katika maji;Kadhalika moyo wa mtu na mwenzake.
20. Kuzimu na Uharibifu havishibi;Wala macho ya wanadamu hayashibi.
21. Kalibu ni kwa fedha, na tanuru kwa dhahabu;Na mtu hujaribiwa kwa sifa zake.
22. Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano;Upumbavu wake hautamtoka.
23. Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako;Na kuwaangalia sana ng’ombe zako.
24. Kwa maana mali haziwi za milele;Na taji je! Yadumu tangu kizazi hata kizazi?
25. Manyasi huchukuliwa, na majani mabichi huonekana,Na maboga ya milimani hukusanyika.
26. Wana-kondoo hufaa kwa mavazi yako;Na mbuzi ni thamani ya shamba