Mit. 27:16-21 Swahili Union Version (SUV)

16. Atakaye kumzuia huyo huuzuia upepo;Na mkono wake wa kuume hukuta mafuta.

17. Chuma hunoa chuma;Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake.

18. Yeye autunzaye mtini atakula matunda yake;Naye amhudumiaye bwana wake ataheshimiwa.

19. Kama uso ufananavyo na uso katika maji;Kadhalika moyo wa mtu na mwenzake.

20. Kuzimu na Uharibifu havishibi;Wala macho ya wanadamu hayashibi.

21. Kalibu ni kwa fedha, na tanuru kwa dhahabu;Na mtu hujaribiwa kwa sifa zake.

Mit. 27