15. Kutona-tona daima siku ya mvua nyingi,Na mwanamke mgomvi ni sawasawa;
16. Atakaye kumzuia huyo huuzuia upepo;Na mkono wake wa kuume hukuta mafuta.
17. Chuma hunoa chuma;Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake.
18. Yeye autunzaye mtini atakula matunda yake;Naye amhudumiaye bwana wake ataheshimiwa.
19. Kama uso ufananavyo na uso katika maji;Kadhalika moyo wa mtu na mwenzake.
20. Kuzimu na Uharibifu havishibi;Wala macho ya wanadamu hayashibi.
21. Kalibu ni kwa fedha, na tanuru kwa dhahabu;Na mtu hujaribiwa kwa sifa zake.
22. Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano;Upumbavu wake hautamtoka.
23. Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako;Na kuwaangalia sana ng’ombe zako.