2. Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake,Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake;Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu.
3. Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda,Na fimbo kwa mgongo wa mpumbavu.
4. Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake;Usije ukafanana naye.
5. Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake;Asije akawa mwenye hekima machoni pake.
6. Apelekaye ujumbe kwa mkono wa mpumbavuHujikata miguu, na kunywa hasara.
7. Miguu yake achechemeaye huwa dhaifu;Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu.
8. Kama mfuko wa vito katika chungu ya mawe;Kadhalika mtu amheshimuye mpumbavu.
9. Kama mwiba uingiao katika mkono wa mlevi;Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu.
10. Fundi stadi hufanyiza vitu vyote;Bali amwajiriye mpumbavu ni kama awaajiriye watu wapitao.
11. Kama vile mbwa arudiavyo matapiko yake;Kadhalika mpumbavu afanya upumbavu tena.
12. Je! Wamwona mtu mwenye hekima machoni pake mwenyewe?Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye.
13. Mtu mvivu husema, Simba yuko njiani,Simba yuko katika njia kuu.