17. Mtu apitaye na kujisumbua kwa ugomvi usio wake;Ni kama mtu ashikaye mbwa kwa masikio yake.
18. Kama mtu mwenye wazimu atupaye mienge,Na mishale, na mauti;
19. Ndivyo alivyo amdanganyaye mwenzake,Na kusema, Je! Sikufanya mzaha tu?
20. Moto hufa kwa kukosa kuni;Na bila mchongezi fitina hukoma.
21. Kama makaa juu ya makaa yanayowaka,Na kama kuni juu ya moto;Ndivyo mtu mgomvi achocheavyo uadui.
22. Maneno ya mchongezi ni kama vitoweo.Nayo hushukia pande za ndani za tumbo.
23. Midomo ijipendekezayo pamoja na moyo mbayaNi kama kigae kilichofunikizwa taka za fedha.
24. Achukiaye huficha chuki kwa midomo yake;Naye huweka akiba ya hila moyoni mwake.
25. Anenapo maneno mazuri usimsadiki;Kwa maana ana machukizo saba moyoni mwake.
26. Ingawa chuki hufunikizwa kwa hila;Uovu wake utadhihirika mbele ya kusanyiko.
27. Achimbaye shimo atatumbukia mwenyewe;Naye abingirishaye jiwe litamrudia.