Mit. 26:1-9 Swahili Union Version (SUV)

1. Kama theluji wakati wa joto, na mvua wakati wa mavuno;Kadhalika heshima haimpasi mpumbavu.

2. Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake,Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake;Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu.

3. Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda,Na fimbo kwa mgongo wa mpumbavu.

4. Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake;Usije ukafanana naye.

5. Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake;Asije akawa mwenye hekima machoni pake.

6. Apelekaye ujumbe kwa mkono wa mpumbavuHujikata miguu, na kunywa hasara.

7. Miguu yake achechemeaye huwa dhaifu;Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu.

8. Kama mfuko wa vito katika chungu ya mawe;Kadhalika mtu amheshimuye mpumbavu.

9. Kama mwiba uingiao katika mkono wa mlevi;Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu.

Mit. 26