1. Kama theluji wakati wa joto, na mvua wakati wa mavuno;Kadhalika heshima haimpasi mpumbavu.
2. Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake,Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake;Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu.
3. Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda,Na fimbo kwa mgongo wa mpumbavu.
4. Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake;Usije ukafanana naye.
5. Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake;Asije akawa mwenye hekima machoni pake.