Mit. 25:13-20 Swahili Union Version (SUV)

13. Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno;Ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwao wamtumao;Kwa maana huwaburudisha bwana zake nafsi zao.

14. Kama mawingu na upepo pasipo mvua;Ndivyo alivyo yeye ajisifiaye karama kwa uongo.

15. Kwa uvumilivu mwingi mkuu husadikishwa;Na ulimi laini huvunja mfupa.

16. Je! Umeona asali? Kula kadiri ya kukutosha;Usije ukashiba na kuitapika.

17. Mguu wako usiingie katika nyumba ya jirani yako ila kwa kiasi;Asije akakukinai na kukuchukia.

18. Mtu amshuhudiaye jirani yake uongoNi nyundo, na upanga, na mshale mkali.

19. Kumtumaini asiye mwaminifu wakati wa taabuNi kama jino lililovunjika, au mguu ulioteguka.

20. Amwimbiaye nyimbo mtu mwenye moyo mzito,Ni kama yeye avuaye nguo wakati wa baridi;Ni kama siki juu ya magadi.

Mit. 25