1. Usiwahusudu watu waovu,Wala usitamani kuwa pamoja nao;
2. Kwa maana moyo wao hufikiri dhuluma,Na midomo yao huongea madhara.
3. Nyumba hujengwa kwa hekima,Na kwa ufahamu huthibitika,
4. Na kwa maarifa vyumba vyake hujazwaVitu vyote vya thamani na vya kupendeza.
5. Mtu mwenye hekima ana nguvu;Naam, mtu wa maarifa huongeza uwezo;
6. Maana kwa mashauri ya akili utafanya vita;Na kwa wingi wa washauri huja wokovu.
7. Kwa mpumbavu hekima haipatikani;Hafumbui kinywa chake langoni.
8. Mtu afikiriye kutenda maovu,Watu watamwita mtundu;
9. Fikira za mpumbavu ni dhambi,Na mwenye mzaha huwachukiza watu.
10. Ukizimia siku ya taabu,Nguvu zako ni chache.
11. Uwaokoe wanaochukuliwa ili wauawe;Nao walio tayari kuchinjwa uwaopoe.
12. Ukisema, Sisi hatukujua hayo;Je! Yeye aipimaye mioyo siye afahamuye?Naye ailindaye nafsi yako siye ajuaye?Je! Hatamlipa kila mtu sawasawa na kazi yake?