12. Elekeza moyo wako kusikiliza mafundisho;Tega masikio yako kusikia maneno ya maarifa.
13. Usimnyime mtoto wako mapigo;Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.
14. Utampiga kwa fimbo,Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu.
15. Mwanangu, kama moyo wako una hekima,Moyo wangu utafurahi, naam, moyo wangu;
16. Naam, viuno vyangu vitafurahi,Midomo yako inenapo maneno mema.
17. Moyo wako usiwahusudu wenye dhambi;Bali mche BWANA mchana kutwa;
18. Maana bila shaka iko thawabu;Na tumaini lako halitabatilika.
19. Sikia, mwanangu, uwe na hekima,Na kuuongoza moyo wako katika njia njema.
20. Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo;Miongoni mwao walao nyama kwa pupa.