1. Utakapoketi kwa chakula pamoja na mtawala,Mwangalie sana yeye aliye mbele yako.
2. Tena ujitie kisu kooni,Kama ukiwa mlafi.
3. Usivitamani vyakula vyake vya anasa;Kwa maana ni vyakula vya hila.
4. Usijitaabishe ili kupata utajiri;Acha kuzitegemea akili zako mwenyewe.
5. Je! Utavikazia macho vile ambavyo si kitu?Maana bila shaka mali hujifanyia mabawa,Kama tai arukaye mbinguni.
6. Usile mkate wa mtu mwenye husuda;Wala usivitamani vyakula vyake vya anasa;