17. Tega sikio lako uyasikie maneno ya wenye hekima, na kuuelekeza moyo wako kwa maarifa yangu;
18. maana ni vizuri kuyahifadhi ndani yako, hali yakithibitika pamoja midomoni mwako.
19. Ili matumaini yako uyaweke kwa BWANA, leo nimekujulisha wewe haya, naam, wewe.
20. Je! Sikukuandikia mambo makuu juu ya mashauri na juu ya maarifa;
21. ili kukujulisha hakika ya maneno ya kweli, uwarudishie wakutumao maneno ya kweli?
22. Usimnyang’anye maskini, kwa kuwa ni maskini;Wala usimdhulumu mtu mnyonge langoni;
23. Kwa sababu BWANA atawatetea;Naye atawateka uhai wao waliowateka.
24. Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi;Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi;
25. Usije ukajifunza njia zake;Na kujipatia nafsi yako mtego.
26. Usiwe mmoja wao wawekao rehani;Au walio wadhamini kwa deni za watu;
27. Kama huna kitu cha kulipa;Kwani ukaondolee kitanda chako chini yako?
28. Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani,Uliowekwa na baba zako.