12. Macho ya BWANA humhifadhi mwenye maarifa;Bali huyapindua maneno ya mtu haini.
13. Mtu mvivu husema, Simba yuko nje;Nitauawa katika njia kuu.
14. Kinywa cha malaya ni shimo refu;Anayechukiwa na BWANA atatumbukia ndani yake.
15. Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto;Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.
16. Yeye awaoneaye maskini ili kuongeza mapato,Naye ampaye tajiri, hupata hasara.
17. Tega sikio lako uyasikie maneno ya wenye hekima, na kuuelekeza moyo wako kwa maarifa yangu;