10. Mtupe nje mwenye dharau, na ugomvi utatoka;Naam, fitina na fedheha zitakoma.
11. Apendaye usafi wa moyo, na neema ya midomo;Mfalme atakuwa rafiki yake.
12. Macho ya BWANA humhifadhi mwenye maarifa;Bali huyapindua maneno ya mtu haini.
13. Mtu mvivu husema, Simba yuko nje;Nitauawa katika njia kuu.
14. Kinywa cha malaya ni shimo refu;Anayechukiwa na BWANA atatumbukia ndani yake.
15. Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto;Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.
16. Yeye awaoneaye maskini ili kuongeza mapato,Naye ampaye tajiri, hupata hasara.