1. Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi;Na neema kuliko fedha na dhahabu.
2. Tajiri na maskini hukutana pamoja;BWANA ndiye aliyewaumba wote wawili.
3. Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha;Bali wajinga huendelea mbele wakaumia.
4. Thawabu ya unyenyekevu ambao ni kumcha BWANANi utajiri, na heshima, nayo ni uzima.
5. Miiba na mitego huwa katika njia ya mshupavu;Yeye aitunzaye nafsi yake atakuwa mbali nayo.
6. Mlee mtoto katika njia impasayo,Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.
7. Tajiri humtawala maskini,Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye.
8. Yeye apandaye uovu atavuna msiba,Na fimbo ya ghadhabu yake itakoma.