1. Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi;Na neema kuliko fedha na dhahabu.
2. Tajiri na maskini hukutana pamoja;BWANA ndiye aliyewaumba wote wawili.
3. Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha;Bali wajinga huendelea mbele wakaumia.
4. Thawabu ya unyenyekevu ambao ni kumcha BWANANi utajiri, na heshima, nayo ni uzima.
5. Miiba na mitego huwa katika njia ya mshupavu;Yeye aitunzaye nafsi yake atakuwa mbali nayo.
6. Mlee mtoto katika njia impasayo,Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.
7. Tajiri humtawala maskini,Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye.