22. Mwenye hekima huupandia mji wao wenye nguvu;Na kuziangusha nguvu za tumaini lao.
23. Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake,Atajilinda nafsi yake na taabu.
24. Mwenye kiburi na kutakabari, jina lake ni mbishi;Hutenda mambo katika majivuno ya kiburi chake.
25. Matakwa yake mtu mvivu humfisha,Kwa maana mikono yake hukataa kufanya kazi.
26. Kuna atamaniye kwa choyo mchana kutwa;Bali mwenye haki hutoa wala hanyimi.
27. Sadaka ya wasio haki ni chukizo;Si zaidi sana ailetapo mwenye nia mbaya!
28. Shahidi wa uongo atapotea;Bali mtu asikiaye atasema maneno yadumuyo.
29. Asiye haki huufanya uso wake kuwa mgumu;Bali mtu mnyofu huzifikiri njia zake.
30. Hapana hekima, wala ufahamu,Wala shauri, juu ya BWANA.