Mit. 21:19-27 Swahili Union Version (SUV)

19. Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika;Kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi.

20. Kuna hazina ya thamani na mafuta katika maskani ya mwenye hekima;Bali mwanadamu aliye mpumbavu huyameza.

21. Aandamaye haki na fadhili,Ataona uhai na haki na heshima.

22. Mwenye hekima huupandia mji wao wenye nguvu;Na kuziangusha nguvu za tumaini lao.

23. Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake,Atajilinda nafsi yake na taabu.

24. Mwenye kiburi na kutakabari, jina lake ni mbishi;Hutenda mambo katika majivuno ya kiburi chake.

25. Matakwa yake mtu mvivu humfisha,Kwa maana mikono yake hukataa kufanya kazi.

26. Kuna atamaniye kwa choyo mchana kutwa;Bali mwenye haki hutoa wala hanyimi.

27. Sadaka ya wasio haki ni chukizo;Si zaidi sana ailetapo mwenye nia mbaya!

Mit. 21