12. Mwenye haki huitafakari nyumba ya mtu mbaya;Jinsi wabaya waangushwavyo wakaangamia.
13. Azibaye masikio yake asisikie kilio cha maskini,Yeye naye atalia, lakini hatasikiwa.
14. Kipawa cha siri hutuliza hasira;Na rushwa bindoni humliza ghadhabu kali.
15. Ni furaha yao wenye haki kutenda hukumu;Lakini ni uharibifu kwao watendao maovu.
16. Mtu aikosaye njia ya busaraAtakaa katika mkutano wao waliokufa.
17. Mtu apendaye anasa atakuwa maskini;Apendaye mvinyo na mafuta hatakuwa tajiri.
18. Mtu asiye haki ni fidia ya wenye haki;Naye afanyaye hila ni badala ya watu wa adili.
19. Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika;Kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi.
20. Kuna hazina ya thamani na mafuta katika maskani ya mwenye hekima;Bali mwanadamu aliye mpumbavu huyameza.
21. Aandamaye haki na fadhili,Ataona uhai na haki na heshima.