Mit. 20:1-9 Swahili Union Version (SUV)

1. Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi;Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.

2. Utisho wa mfalme ni kama ngurumo ya simba;Amkasirishaye huitendea dhambi nafsi yake.

3. Mtu kujitenga na ugomvi ni heshima kwake;Bali kila mpumbavu ataka kugombana.

4. Mtu mvivu hataki kulima wakati wa baridi;Hivyo wakati wa mavuno ataomba, hana kitu.

5. Mashauri ya moyoni ni kama kilindi;Lakini mtu mwenye ufahamu atayateka.

6. Wanadamu hutangaza kila mtu hisani yake mwenyewe;Bali mtu aliye mwaminifu, ni nani awezaye kumpata?

7. Mwenye haki aendaye katika unyofu wake,Watoto wake wabarikiwa baada yake.

8. Mfalme aketiye katika kiti cha hukumu,Huyapepeta mabaya yote kwa macho yake.

9. Nani awezaye kusema, Nimesafisha moyo wangu;Nimetakasika dhambi yangu?

Mit. 20