3. Naam, ukiita busara,Na kupaza sauti yako upate ufahamu;
4. Ukiutafuta kama fedha,Na kuutafutia kama hazina iliyositirika;
5. Ndipo utakapofahamu kumcha BWANA,Na kupata kumjua Mungu.
6. Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima;Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu;
7. Huwawekea wanyofu akiba ya hekima kamili;Yeye ni ngao kwao waendao kwa ukamilifu;
8. Apate kuyalinda mapito ya hukumu,Na kuhifadhi njia ya watakatifu wake.
9. Ndipo utakapofahamu haki na hukumu,Na adili, na kila njia njema.
10. Maana hekima itaingia moyoni mwako,Na maarifa yatakupendeza nafsi yako;
11. Busara itakulinda;Ufahamu utakuhifadhi.
12. Ili kukuokoa na njia ya uovu,Na watu wanenao yaliyopotoka;
13. Watu waziachao njia za unyofu,Ili kuziendea njia za giza;