18. Maana nyumba yake inaelekea mauti,Na mapito yake yanakwenda kwenye wafu.
19. Katika hao wamwendeao harudi hata mmoja,Wala hawazifikilii njia za uzima.
20. Ili upate kwenda katika njia ya watu wema,Na kuyashika mapito ya wenye haki.
21. Maana wanyofu watakaa katika nchi,Na wakamilifu watadumu ndani yake.