Mit. 19:23-27 Swahili Union Version (SUV)

23. Kumcha BWANA huelekea uhai;Atakaa ameshiba; hatajiliwa na ubaya.

24. Mtu mvivu hutia mkono wake sahanini;Ila hataki hata kuupeleka kinywani pake.

25. Mpige mwenye mzaha, na mjinga atapata busara;Mwonye mwenye ufahamu, naye atatambua maarifa.

26. Apotezaye mali za babaye na kumfukuza mamaye,Ni mwana aaibishaye, na kuleta lawama.

27. Mwanangu, acha kusikia mafundisho,Ukitaka tu kuyaasi maneno ya maarifa.

Mit. 19