Mit. 19:20-28 Swahili Union Version (SUV)

20. Sikiliza mashauri, ukapokee mafundisho,Upate kuwa na hekima siku zako za mwisho.

21. Mna hila nyingi moyoni mwa mtu;Lakini shauri la BWANA ndilo litakalosimama.

22. Haja ya mwanadamu ni hisani yake;Ni afadhali maskini kuliko mwongo.

23. Kumcha BWANA huelekea uhai;Atakaa ameshiba; hatajiliwa na ubaya.

24. Mtu mvivu hutia mkono wake sahanini;Ila hataki hata kuupeleka kinywani pake.

25. Mpige mwenye mzaha, na mjinga atapata busara;Mwonye mwenye ufahamu, naye atatambua maarifa.

26. Apotezaye mali za babaye na kumfukuza mamaye,Ni mwana aaibishaye, na kuleta lawama.

27. Mwanangu, acha kusikia mafundisho,Ukitaka tu kuyaasi maneno ya maarifa.

28. Shahidi asiyefaa kitu hudhihaki hukumu,Na vinywa vya wasio haki humeza uovu.

Mit. 19