20. Sikiliza mashauri, ukapokee mafundisho,Upate kuwa na hekima siku zako za mwisho.
21. Mna hila nyingi moyoni mwa mtu;Lakini shauri la BWANA ndilo litakalosimama.
22. Haja ya mwanadamu ni hisani yake;Ni afadhali maskini kuliko mwongo.
23. Kumcha BWANA huelekea uhai;Atakaa ameshiba; hatajiliwa na ubaya.
24. Mtu mvivu hutia mkono wake sahanini;Ila hataki hata kuupeleka kinywani pake.
25. Mpige mwenye mzaha, na mjinga atapata busara;Mwonye mwenye ufahamu, naye atatambua maarifa.