Mit. 19:2-13 Swahili Union Version (SUV)

2. Tena si vizuri nafsi ya mtu ikose maarifa;Naye afanyaye haraka kwa miguu hutenda dhambi.

3. Upumbavu wa mtu hupotosha njia yake;Na moyo wake hununa juu ya BWANA.

4. Utajiri huongeza rafiki wengi;Bali maskini hutengwa na rafiki yake.

5. Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa;Wala asemaye uongo hataokoka.

6. Watu wengi watamsihi mkuu ili awafadhili;Na kila mtu ni rafiki yake atoaye tunu.

7. Ndugu zote wa maskini humchukia;Jinsi gani rafiki zake huzidi kujitenga naye!Huwafuata kwa maneno, lakini wametoweka.

8. Apataye hekima hujipenda nafsi yake;Ashikaye ufahamu atapata mema.

9. Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa;Naye asemaye uongo ataangamia.

10. Maisha ya anasa hayampasi mpumbavu;Sembuse mtumwa awatawale wakuu.

11. Busara ya mtu huiahirisha hasira yake;Nayo ni fahari yake kusamehe makosa.

12. Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba;Bali hisani yake kama umande juu ya majani.

13. Mwana mpumbavu ni msiba kwa babaye;Na ugomvi wa mke kama kutona-tona daima.

Mit. 19