7. Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake,Na midomo yake ni mtego wa nafsi yake.
8. Maneno ya mchongezi ni kama vitoweo;Nayo hushukia pande za ndani za tumbo.
9. Yeye naye aliye mvivu katika kazi yake,Ni ndugu yake aliye mharabu.
10. Jina la BWANA ni ngome imara;Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.
11. Mali ya mtu tajiri ni mji wake wa nguvu;Ni kama ukuta mrefu katika mawazo yake.
12. Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna;Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.
13. Yeye ajibuye kabla hajasikia,Ni upumbavu na aibu kwake.
14. Roho ya mtu itastahimili udhaifu wake;Bali roho iliyovunjika nani awezaye kuistahimili?
15. Moyo wa mwenye busara hupata maarifa;Na sikio la mwenye hekima hutafuta maarifa.
16. Zawadi ya mtu humpatia nafasi;Humleta mbele ya watu wakuu.