1. Ajitengaye na wenzake hutafuta matakwa yake mwenyewe;Hushindana na kila shauri jema.
2. Mpumbavu hapendezwi na ufahamu;Ila moyo wake udhihirike tu.
3. Ajapo asiye haki, huja dharau pia;Na pamoja na aibu huja lawama.
4. Maneno ya kinywa cha mtu ni kama maji ya vilindi;Kijito kibubujikacho; chemchemi ya hekima.
5. Kukubali uso wake asiye haki si vizuri;Wala kumpotosha mwenye haki hukumuni.
6. Midomo ya mpumbavu huingia katika fitina,Na kinywa chake huita mapigo.
7. Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake,Na midomo yake ni mtego wa nafsi yake.
8. Maneno ya mchongezi ni kama vitoweo;Nayo hushukia pande za ndani za tumbo.
9. Yeye naye aliye mvivu katika kazi yake,Ni ndugu yake aliye mharabu.
10. Jina la BWANA ni ngome imara;Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.
11. Mali ya mtu tajiri ni mji wake wa nguvu;Ni kama ukuta mrefu katika mawazo yake.