Mit. 17:9-18 Swahili Union Version (SUV)

9. Afunikaye kosa hutafuta kupendwa;Bali yeye akashifuye neno hutenga rafiki.

10. Lawama hupenya moyoni mwa mwenye ufahamu,Kuliko mapigo mia moyoni mwa mpumbavu.

11. Mtu mwovu hataki neno ila kuasi tu;Kwa hiyo mjumbe mkali atatumwa kwake.

12. Afadhali mtu akutwe na dubu aliyenyang’anywa watoto wake,Kuliko na mpumbavu katika upumbavu wake.

13. Yeye arudishaye mabaya badala ya mema,Mabaya hayataondoka nyumbani mwake.

14. Mwanzo wa ugomvi ni kama kutoboa penye maji;Basi acheni ugomvi kabla haujafurika.

15. Yeye asemaye kwamba asiye haki ana haki;naye asemaye kwamba mwenye haki hana haki;Hao wote wawili ni chukizo kwa BWANA.

16. Nini maana yake, mpumbavu kuwa na fedha mkononi mwake ya kununulia hekima,Ikiwa hana moyo wa ufahamu?

17. Rafiki hupenda sikuzote;Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu.

18. Aliyepungukiwa na akili hupana mkono na mtu;Na kuwa mdhamini mbele ya mwenzake.

Mit. 17