18. Aliyepungukiwa na akili hupana mkono na mtu;Na kuwa mdhamini mbele ya mwenzake.
19. Apendaye ugomvi hupenda dhambi;Auinuaye sana mlango wake hutafuta uharibifu.
20. Mtu mwenye moyo wa ukaidi hatapata mema;Na mwenye ulimi wa upotofu huanguka katika misiba.
21. Azaaye mpumbavu ni kwa huzuni yake mwenyewe;Wala baba wa mpumbavu hana furaha.
22. Moyo uliochangamka ni dawa nzuri;Bali roho iliyopondeka huikausha mifupa.
23. Asiye haki hutoa rushwa kifuani,Ili kuzipotosha njia za hukumu.
24. Hekima huwa machoni pake mwenye ufahamu;Bali macho ya mpumbavu huwa katika ncha za dunia.