Mit. 17:13-27 Swahili Union Version (SUV)

13. Yeye arudishaye mabaya badala ya mema,Mabaya hayataondoka nyumbani mwake.

14. Mwanzo wa ugomvi ni kama kutoboa penye maji;Basi acheni ugomvi kabla haujafurika.

15. Yeye asemaye kwamba asiye haki ana haki;naye asemaye kwamba mwenye haki hana haki;Hao wote wawili ni chukizo kwa BWANA.

16. Nini maana yake, mpumbavu kuwa na fedha mkononi mwake ya kununulia hekima,Ikiwa hana moyo wa ufahamu?

17. Rafiki hupenda sikuzote;Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu.

18. Aliyepungukiwa na akili hupana mkono na mtu;Na kuwa mdhamini mbele ya mwenzake.

19. Apendaye ugomvi hupenda dhambi;Auinuaye sana mlango wake hutafuta uharibifu.

20. Mtu mwenye moyo wa ukaidi hatapata mema;Na mwenye ulimi wa upotofu huanguka katika misiba.

21. Azaaye mpumbavu ni kwa huzuni yake mwenyewe;Wala baba wa mpumbavu hana furaha.

22. Moyo uliochangamka ni dawa nzuri;Bali roho iliyopondeka huikausha mifupa.

23. Asiye haki hutoa rushwa kifuani,Ili kuzipotosha njia za hukumu.

24. Hekima huwa machoni pake mwenye ufahamu;Bali macho ya mpumbavu huwa katika ncha za dunia.

25. Mwana mpumbavu ni huzuni kwa babaye,Na uchungu kwa mamaye aliyemzaa.

26. Tena kumwadhibu mwenye haki si vizuri;Wala si kwema kuwapiga wakuu kwa unyofu wao.

27. Azuiaye maneno yake ni mwenye maarifa;Na mwenye roho ya utulivu ana busara.

Mit. 17