22. Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwake aliye nao;Bali kufundishwa kwa wapumbavu ni upuzi wao.
23. Moyo wake mwenye hekima hufundisha kinywa chake;Huzidisha elimu ya midomo yake.
24. Maneno yapendezayo ni kama sega la asali;Ni tamu nafsini, na afya mifupani.
25. Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu;Lakini mwisho wake ni njia za mauti.
26. Nafsi yake mfanya kazi hujifanyia kazi;Maana kinywa chake humtia bidii.
27. Mtu asiyefaa kitu huchimba shimo la madhara;Katika midomo yake mna moto uteketezao.
28. Mtu mshupavu huondokesha fitina;Na mchongezi huwafarakanisha rafiki.
29. Mtu mkali humshawishi mwenzake;Humwongoza katika njia isiyo njema.
30. Afumbaye macho, kusudi lake ni kuwaza yaliyopotoka;Aikazaye midomo yake hutokeza mabaya.
31. Kichwa chenye mvi ni taji ya utukufu,Kama kikionekana katika njia ya haki.
32. Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa;Na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji.