5. mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia.
6. Kufahamu mithali na kitendawili, na maneno ya wenye hekima na mafumbo yao.
7. Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.
8. Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako,Wala usiiache sheria ya mama yako,
9. Kwa maana hayo yatakuwa kilemba cha neema kichwani pako,Na mikufu shingoni mwako.