22. Enyi wajinga, hata lini mtapenda ujinga?Na wenye dharau kupenda dharau yao,Na wapumbavu kuchukia maarifa?
23. Geukeni kwa ajili ya maonyo yangu;Tazama, nitawamwagia roho yangu,Na kuwajulisheni maneno yangu.
24. Kwa kuwa nimeita, nanyi mkakataa;Nimeunyosha mkono wangu, asiangalie mtu;
25. Bali mmebatilisha shauri langu,Wala hamkutaka maonyo yangu;
26. Mimi nami nitacheka siku ya msiba wenu,Nitadhihaki hofu yenu ifikapo;
27. Hofu yenu ifikapo kama tufani,Na msiba wenu ufikapo kama kisulisuli,Dhiki na taabu zitakapowafikia.
28. Ndipo watakaponiita, lakini sitaitika;Watanitafuta kwa bidii, wasinione.
29. Kwa kuwa walichukia maarifa,Wala hawakuchagua kumcha BWANA.
30. Hawakukubali mashauri yangu,Wakayadharau maonyo yangu yote.
31. Kwa hiyo watakula matunda ya njia yao,Watashiba mashauri yao wenyewe.