Mik. 5:9-11 Swahili Union Version (SUV)

9. Mkono wako na uinuliwe juu ya adui zako, na adui zako wote wakauliwe mbali.

10. Kisha itakuwa katika siku hiyo, asema BWANA, nitawakatilia mbali farasi zako watoke kati yako, nami nitayaharibu magari yako ya vita;

11. nami nitaikatilia mbali miji ya nchi yako, na ngome zako zote nitaziangusha;

Mik. 5