Mik. 5:7-13 Swahili Union Version (SUV)

7. Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya kabila nyingi mfano wa umande utokao kwa BWANA, mfano wa manyunyu katika manyasi; yasiyomngojea mtu, wala kuwakawilia wanadamu.

8. Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya mataifa, kati ya kabila nyingi, mfano wa simba kati ya wanyama wa msituni, kama mwana-simba kati ya makundi ya kondoo, ambaye, akiwa anapita katikati, hukanyaga-kanyaga na kurarua-rarua, wala hakuna wa kuokoa.

9. Mkono wako na uinuliwe juu ya adui zako, na adui zako wote wakauliwe mbali.

10. Kisha itakuwa katika siku hiyo, asema BWANA, nitawakatilia mbali farasi zako watoke kati yako, nami nitayaharibu magari yako ya vita;

11. nami nitaikatilia mbali miji ya nchi yako, na ngome zako zote nitaziangusha;

12. nami nitakatilia mbali uchawi, usiwe mkononi mwako; wala hutakuwa tena na watu wenye kutabana;

13. nami nitakatilia mbali sanamu zako na nguzo zako, zitoke kati yako; wala hutaiabudu tena kazi ya mikono yako.

Mik. 5