12. nami nitakatilia mbali uchawi, usiwe mkononi mwako; wala hutakuwa tena na watu wenye kutabana;
13. nami nitakatilia mbali sanamu zako na nguzo zako, zitoke kati yako; wala hutaiabudu tena kazi ya mikono yako.
14. Nami nitayang’oa maashera yenu, yasiwe kati yako; nami nitaiangamiza miji yako.
15. Nami nitajilipiza kisasi katika hasira na ghadhabu juu ya mataifa wasiosikiliza.