11. Na sasa mataifa mengi wamekusanyika juu yako, wasemao, Na atiwe unajisi; macho yetu na yaone shari ya Sayuni.
12. Lakini wao hawayajui mawazo ya BWANA, wala hawafahamu shauri lake; kwa maana amewakusanya kama miganda sakafuni.
13. Haya, simama upure, Ee binti Sayuni; kwa maana nitafanya pembe yako kuwa chuma, na kwato zako kuwa shaba; nawe utaponda-ponda mataifa mengi, na faida yao utaiweka wakfu kwa BWANA, na mali zao kwa BWANA wa dunia yote.