Mhu. 7:7-21 Swahili Union Version (SUV)

7. Kweli jeuri humpumbaza mwenye hekima,Na rushwa huuharibu ufahamu.

8. Heri mwisho wa neno kuliko mwanzo wake,Na mvumilivu rohoni kuliko mwenye roho ya kiburi.

9. Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako,Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.

10. Usiseme, Kwani siku za kale kupita siku hizi?Maana si kwa hekima uulizavyo neno hilo.

11. Hekima ni njema, mfano wa urithi;Naam, nayo ni bora kwao walionao jua.

12. Kwa maana hekima ni ulinzi, kama vile fedha ilivyo ulinzi; na ubora wa maarifa ni ya kwamba hekima humhifadhi yeye aliye nayo.

13. Tafakari vema kazi yake Mungu; kwa sababu ni nani awezaye kukinyosha kitu kile alichokipotosha yeye?

14. Siku ya kufanikiwa ufurahi,Na siku ya mabaya ufikiri. Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambamba na hiyo ya pili, ili mwanadamu asipate kulijua neno lo lote litakalofuata baada yake.

15. Mambo hayo yote nimeyaona mimi katika siku za ubatili wangu, yuko mwenye haki apoteaye katika haki yake, yuko na mtu mwovu azidishaye maisha yake katika udhalimu wake.

16. Usiwe na haki kupita kiasi;Wala usijiongezee hekima mno;Kwani kujiangamiza mwenyewe?

17. Usiwe mwovu kupita kiasi;Wala usiwe mpumbavu;Kwani ufe kabla ya wakati wako?

18. Ni vizuri kwamba ulishike neno hilo; naam, hata kwa neno hilo tena usiuondoe mkono wako; kwa kuwa mtu yule amchaye Mungu atatoka katika hayo yote.

19. Hekima ni nguvu zake mwenye hekima,Zaidi ya wakuu kumi waliomo mjini.

20. Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi.

21. Tena, usitie moyoni mwako maneno yote yaliyosemwa; usije ukamsikia mtumwa wako mwenyewe ali anakutukana.

Mhu. 7