Mhu. 1:11-16 Swahili Union Version (SUV)

11. Hakuna kumbukumbu lo lote la vizazi vilivyotangulia; wala hakutakuwa na kumbukumbu lo lote la vizazi vitakavyokuja, miongoni mwao wale watakaofuata baadaye.

12. Mimi, Mhubiri, nalikuwa Mfalme wa Israeli katika Yerusalemu.

13. Nikatia moyo wangu ili kuyatafuta yote yanayotendeka chini ya mbingu, na kuyavumbua kwa hekima; ni taabu kubwa ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake.

14. Nimeziona kazi zote zifanywazo chini ya jua; na, tazama, mambo yote ni ubatili na kujilisha upepo.

15. Yaliyopotoka hayawezi kunyoshwa,Wala yasiyokuwapo hayahesabiki.

16. Nikatafakari nikisema, Nimejipatia hekima nyingi kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; naam, moyo wangu umeona kwa wingi hekima na maarifa.

Mhu. 1