Mdo 9:16-28 Swahili Union Version (SUV)

16. Maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu.

17. Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu.

18. Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa;

19. akala chakula, na kupata nguvu.Akawa huko siku kadha wa kadha pamoja na wanafunzi walioko Dameski.

20. Mara akamhubiri Yesu katika masinagogi, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu.

21. Na wote waliosikia wakashangaa, wakasema, Siye huyu aliyewaharibu walioliitia Jina hili huko Yerusalemu? Na hapa alikuwa amekuja kwa kusudi hilo, awafunge na kuwapeleka kwa wakuu wa makuhani?

22. Sauli akazidi kuwa hodari, akawatia fadhaa Wayahudi waliokaa Dameski, akithibitisha ya kuwa huyu ndiye Kristo.

23. Hata siku nyingi zilipopita, Wayahudi wakafanya shauri ili wamwue;

24. lakini hila yao ikajulikana na Sauli. Wakamvizia malangoni mchana na usiku wapate kumwua.

25. Wanafunzi wake wakamtwaa usiku wakamshusha ukutani, wakimtelemsha katika kapu.

26. Na Sauli alipofika Yerusalemu, alijaribu kujiunga na wanafunzi, nao walikuwa wakimwogopa wote, wasisadiki ya kuwa yeye ni mwanafunzi.

27. Lakini Barnaba akamtwaa, akampeleka kwa mitume, akawaeleza jinsi alivyomwona Bwana njiani, na ya kwamba alisema naye, na jinsi alivyohubiri kwa ushujaa katika Dameski kwa jina la Yesu.

28. Naye akawa pamoja nao katika Yerusalemu akiingia na kutoka.

Mdo 9