18. wakawakamata mitume wakawaweka ndani ya gereza;
19. lakini malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema,
20. Enendeni mkasimame hekaluni mkawaambie watu maneno yote ya Uzima huu.
21. Nao waliposikia wakaenda alfajiri hekaluni, wakaanza kufundisha.Akaja Kuhani Mkuu nao waliokuwa pamoja naye, wakawakutanisha watu wa baraza, na wazee wote wa wana wa Israeli, wakatuma watu gerezani ili wawalete.