Mdo 27:32-34 Swahili Union Version (SUV)

32. Basi askari wakazikata kamba za mashua, wakaiacha ianguke.

33. Na kulipokuwa kukipambauka Paulo akawasihi wote wale chakula, akisema, Leo ni siku ya kumi na nne kungoja na kufunga, hamkula kitu cho chote.

34. Basi nawasihi mle chakula, maana itakuwa kwa wokovu wenu; kwa maana hapana hata unywele wa kichwa cha mmoja wenu utakaopotea.

Mdo 27