2. Naye alipoitwa, Tertulo akaanza kumshitaki, akisema,Kwa kuwa mnapata amani nyingi chini yako, Feliki mtukufu, na kwa maangalizi yako mambo mabaya yanatengenezwa kwa ajili ya taifa hili,
3. basi tunayapokea kila wakati na kila mahali, kwa shukrani yote.
4. Lakini nisikuudhi zaidi, nakusihi utusikilize maneno machache kwa fadhili zako.
5. Kwa maana tumemwona mtu huyu mkorofi, mwanzilishi wa fitina katika Wayahudi wote duniani, tena ni kichwa cha madhehebu ya Wanazorayo.
6. Na tena alijaribu kulitia hekalu unajisi; tukamkamata; [tukataka kumhukumu kwa sheria yetu.
7. Lakini Lisia jemadari akafika akamwondoa mikononi mwetu kwa nguvu,
8. Akawaamuru wale waliomshitaki waje kwako.] Wewe mwenyewe kwa kumwuliza-uliza utaweza kupata habari ya mambo yale yote tunayomshitaki sisi.
9. Wayahudi nao wakamshitaki, wakisema ya kuwa ndivyo yalivyo.
10. Na liwali alipompungia mkono ili anene, Paulo akajibu, Kwa kuwa ninajua ya kwamba wewe umekuwa mwamuzi wa taifa hili kwa muda wa miaka mingi, najitetea mwenyewe kwa moyo wa furaha.